OMG! THIS GUY MIGHT BE SILENCED SOON!!! JICHO PEVU’S MOHAMMED ALI REVEALS THE REAL REASON WHY KDF WENT IN SOMALIA TO FIGHT AL SHABAAB CONTRARY TO POPULAR BELIEF TERRORISTS WERE ATTACKING KENYA! (FULL DETAILS)
Ni kwa nini vijana wetu wauawe kinyama kila kukicha kwa ajili ya makosa ya marekani? Kuingia kwa wanajeshi wa Kenya Somalia kulitokana na kutekwa nyara kwa ajuza mmoja mtalii huko Lamu na Alshabab. Jeshi liliamua kuingia Somalia kwa sababu za ajuza huyo na wala sio wakenya wanaouawa na kutekwa nyara kila mara na Alshabab.


Tamaa ya pesa pia imechangia pakubwa. Yaani wanasiasa na baadhi ya wakuu wa jeshi waliokuwa hapo awali waliona ni vyema kula pesa za wanajeshi hao huku wao wakihangaika kutulinda sisi. Hakika jeshi limegeuzwa na kuwa kama polisi. Hii sio jeshi ya Daniel Toroitich Arap Moi tuliyokuwa tukiiheshimu na kuienzi.

Wakuu wa jeshi wamekuwa wakabila wakubwa wanaojiingiza kwa mambo ya kisiasa. Uhuru Kenyatta warudishe ndugu na dada zetu nyumbani maana tumechoka kulia. Kama amerika ina shida, waende wao wakapigane nao. El Adde mlitudang’anya eti mliwashambulia kabla ya Alshabab kutoa kanda ya video na kutuonyesha jinsi ambavyo waliwaangamiza watoto wetu.

Hii ya ijumaa iliyopita mmetudang’anya lakini kwa vile jeshi pia limeanza tabia za polisi wakenya watasubiri kuona kanda ya Alshabab maana hawaamini serikali yao. Mwisho kabisa kama unaona ni uzalendo kwa wao kubakia naomba uwatume vijana wako, kila waziri ndani ya serikali yako atume vijane wake, mkuu wa jeshi atume kijana wake na hao wanasiasa wanaopayuka kila kukicha ndani ya bunge, seneti na kupasisha mijadala za kitoto pia watume watoto zao.

Mkifanya hivyo nitajua ni ukenya na uzalendo nami pia nitajitolea kuungana nao kulinda taifa langu Kenya,”
Mohammed Ali wrote in part.
PAGE: 1, 2, 
ALSO READ: WTH? MORTUARY ATTENDANTS STORM CEMETERY DURING FUNERAL & SEIZE BODY AFTER FAILURE TO PAY MORTUARY BILL (SEE SHOCKING PHOTOS AND VIDEO)
SEE HERE
Advertisemen

Related Posts